WANAOJIUZULU NA KUHAMA CHAMA TUNAWATAKIA KILA LA KHERI

0
33

WANAOJIUZULU NA KUHAMA CHAMA TUNAWATAKIA KILA LA KHERI, HIYO NI HAKI YAO KWA MUJIBU WA KATIBA YA CUF IBARA YA 117(1):

CUF HAINA CHEO CHA MWANASHERIA MKUU WA CHAMA, ALIYETIWA BEI ASIJIKWEZE KUTAKA KUJINENEPESHA MNADANI:

HOJA WANAZOZITOA HAZINA MASHIKO ZAIDI YA KHOFU ZAO NA KUTANGULIZA MASLAHI BINAFSI KWA KUTIWA BEI:

THE CIVIC UNITED FRONT
(CUF–Chama Cha Wananchi)

TAARIFA KWA UMMA

TAREHE 19 AUGUST, 2018

KUMEZUKA TAHARUKI kwa wanachama wetu na Watanzania wapenda Mabadiliko nchini kufuatia baadhi ya Viongozi wa Chama kwa nafasi za Kiserikali [madiwani na Wabunge] kujiuzulu nafasi zao na kujiunga na CCM. HAKUNA SABABU YA KUTAHARUKI ZAIDI NI KUWAONEA HURUMA KWA SABABU WAMEKUBAKI KUJIVUNJIA HESHIMA ZAO MBELE YA JAMII ILIYOWAAMINI NA KUWA WATUMWA WA KIFIKRA.

MSIMAMO WA CUF KWA SASA NI KAMA IFUATAVYO;

1. Viongozi wanaojiuzulu wanatekeleza Haki yao ya Kikatiba kwa mujibu wa katiba ya CUF ibara ya 117(1) INGAWA hoja wanazozitoa hazina mashiko wala mantiki ya maana zaidi ya khofu zao na kutanguliza maslahi binafsi kwa kuonekana dhahiri kuwa kujiuzulu kwako kumesukumwa na BIASHARA HARAMU-wametiwa bei [Political Corruption]. CUF haina pingamizi kwa Kiongozi au mwanachama yeyote yule pale atakapoona ameshindwa kusimamia Malengo na Madhumuni ya Chama kujiondoa ndani ya Chama. wakati mwingine huwa ni fursa zuri zaidi ya kutupa nafasi ya kujipanga upya kwa kuwa na wapambanaji sahihi katika nafasi husika.

2. CUF haina cheo cha Mwanasheria Mkuu wa Chama kwa mujibu wa Katiba wala kanuni za Chama, Hashimu Mziray ni Afisa wa Kurugenzi ya Haki za Binaadamu na Sheria. Akiwa chini ya Mkurugenzi wake Mhe. Kulthum Mchuchuli. Kurugenzi ina maafisa wawili; Afisa wa Haki za Binaadamu [Mhe.Mohamed Mluya] na Afisa wa Sheria [alikuwa Hashimu Mziray], nadhani alieleza vile ili ionekane kama vile yeye yupo hadhi sawa na Tundu Lissu ili bei yake iwe nono mnadani. HAPANA. Taarifa aliyoitoa si ya sawasawa. Mziray ni wakili wa kujitegemea akiwa na ofisi yake Buguruni kwa Mnyamani ikiitwa Haki Associates Advocates. Kama CUF ingelikuwa na Cheo hicho basi angepewa Taha Taslima au Abubakar Khamis[Hawa ni Ma-senior katika Sheria]. Hata hivyo tunamshukuru kwa mchango wake wa kukisaidia Chama pale tulipokuwa pamoja nae.

3. Kuhusu Kesi/mashauri ya Chama yaliyopo mahakamani, Je kwa kuondoka Wakili Mziray Chama kimeathirika? HAPANA. Kesi zote zenye umuhimu mkubwa kwa Chama zinasimamiwa na Wasomi Mawakili Juma Nassoro, Mhe. Halfani Daimu, Mhe. Fatma Karume, na Mhe. Kabe Mpare Mpoki. Hawa ndio mawakili walioaminiwa na Chama na kukabidhiwa Mashauri haya ikiwemo Shauri la RITA [13/2017, RUZUKU [80/2017 na 68/2017], Uhalali wa Lipumba na Msajili Mutungi [23/2016] na suala hili lilifanyika makhsusi kutokana na kuona kuwa Wakili Mziray bado ni mchanga kisheria. [Junior Lawyer]. Hata shauri la madiwani wa Tanga 3 waliodaiwa kuvuliwa uanachama na Lipumba mwezi July, 2018 linasimamiwa na Wasomi Mawakili Juma Nassoro na Mhe. Halfani Daimu.

4. Kutokana na kadhia hii Chama kitafanya vikao vyake vya Kitaifa [Kamati ya Utendaji ya Taifa na Baraza Kuu la Uongozi la Taifa] ili kufanya tathmini ya pamoja na kuweka mikakati thabiti ya kuendeleza mapambano ya kisiasa, kukilinda Chama na kujaza nafasi wazi za Uongozi zilizokuwepo.

5. Mashauri yetu–CUF yanaendelea kesho Tarehe 20/8/2018 na shauri la RITA lililopangwa Tarehe 16/8/2018 litatajwa tena Tarehe 23/8/2018 na Shauri la Wabunge Viti Maalumu litasikilizwa Tarehe 5/9/2018. Aidha, Shauri namba No. 30/2018
na Shauri No. 2/2018 Madiwani wa CUF Tanga limepangwa Tarehe 29/8/2018.

TUWATOWE HOFU WANACUF, WAPENZI, NA WAPENDA MABADILIKO WOTE NCHINI, KWAMBA CUF NA VIONGOZI WAKE MAKINI WATAENDELEA KUSIMAMA IMARA KUTETEA NA KUPIGANIA MASLAHI MAPANA YA CHAMA CHA CUF NA TAIFA KWA UJUMLA KWA KUENDELEZA MADAI YA HAKI, UHURU, USAWA, DEMOKRASIA NA MABADILIKO MAKUBWA YA KISIASA NA KIUCHUMI NCHINI.

TUSIPOTEZE MUDA WETU KUWAJADILI WASALITI WA MAPAMBANO YETU WALIOAMUA KUTANGULIZA MASLAHI YAO BINAFSI NA KUAMUA KUTAFUTA FURSA ZA AJIRA SERIKALINI. WAPUUZWE KWA KIWANGO KILEKILE CHA USALITI WAO.

HAKI SAWA KWA WOTE

Imetolewa na kurugenzi ya Habari CUF-Taifa;

MBARALA MAHARAGANDE
NAIBU MKURUGENZI-NMHUMU

maharagande@gmail.com
Tigo-0715 062 577, Voda -0767 062 577