Sala ya Eid kusaliwa Makunduchi

0
38

August 21, 2018

NA MWANAJUMA MMANGA

SALA ya Idd El-Hajj kitaifa, inatarajiwa kusaliwa katika kijiji cha Makunduchi Wilaya ya Kusini Mkoa wa Kusini Unguja.

Ofisa shughuli za hijja katika Kamisheni ya Wakfu Maliamana Zanzibar, Hassan Ali Kombo, aliyasema hayo wakati akizungumza na mwandishi wa habari hizi.

Alisema sala hiyo itasaliwa katika uwanja wa mpira wa Jamhuri na kama kutanyesha mvua itasaliwa msikiti wa Mtegani.

Alisema sala hiyo itafuatiwa na baraza la Eid, litakalofanyika katika kijiji jirani cha Kizimkazi Mikunguni, ambapo wageni mbali mbali wakiongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohamed Shein, watashiriki.

Alisema wengine wanaotarajiwa kuhudhuria baraza hilo ni Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Alisema matayarisho yamekamilika, hivyo aliwaomba wananchi wa mkoa huo kujitokeza kwa wingi katika sala hiyo.

Zanzibarleo