Uzalishaji wa dhahabu wapungua Tanzania

0
30
By Sharon Sauwa, Mwananchi [email protected]

Dodoma. Serikali ya Tanzania imesema mwaka 2018 uzalishaji wa dhahabu nchini ulipungua kwa asilimia 9.6.

Hayo yamo katika taarifa ya hali ya uchumi ya mwaka 2018 iliyowasilishwa bungeni na Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango leo Alhamisi, Juni 13 2019.

Amesema mwaka 2018 uzalishaji wa dhahabu ulikuwa kilo 39,304 ukipungua kutoka kilo 43,489 zilizozalishwa mwaka 2017.

“Upungufu huo ulitokana na mgodi wa Bulyanhulu kutozalisha dhahabu katika uwezo wake kwa kuendelea kuzalisha dhahabu kutoka kwenye marudio,”amesema.

Amesema thamani ya mauzo ya dhahabu nje ya nchi ilikuwa Dola za Marekani 1454.88 milioni ikilinganishwa na Dola za Marekani 1636.57 milioni mwaka 2017, sawa na upungufu wa asilimia 11.1.

“Hii ilitokana na kuendelea kupungua kwa kiasi cha dhahabu ghafi kilichouzwa nje ya nchi,”amesema.

Source: mwananchi