Amkata mumewe uume kudai unyumba

0
49

Kampala. Mwanamume mmoja wilayani Apac nchini Uganda, Moses Okot  (46) anauguza jeraha baada ya mkewe kumkata uume kwa madai ya kukosa unyumba.

Okot, ambaye ni mkulima amelieleza gazeti la Daily Monitor kuwa siku ya tukio Jumapili Juni 30 mkewe Beatrice Acen (35) alirudi nyumbani amelewa na kumkata uume wake.

“Niliporudi kutoka kuwinda kama saa 1 usiku, mke wangu hakuepo nyumbani. Binti yangu akanipa chakula na baada ya kula nikaenda kulala. Mke wangu alirudi karibu saa 4 usiku na kufoka nimfungulie,” alisema okot.

“Nilikuwa tayari nimelala usingizi. Nilihisi maumivu kidogo yaliyoniamsha na nilipojikuta chupi yangu imelowana damu,” aliongeza.

Okot aliendelea kusimulia “mke wangu amekuwa anakuja nyumbani amelewa sana. Kama mwanamume nilishindwa kuvumilia hali ile, niliamua kumnyima unyumba nikiamini atajirudi. Amekuwa akidai unyumba.”

Okot na Acen wameishi pamoja kwa zaidi ya miaka 10 na wamepata pamoja watoto watano.

Hata hivyo, mwenyekiti wa Kijiji cha Amin B, amesema wanandoa hao wamekuwa wanagombana mara kwa mara. Amethibitisha kuwa mara kadhaa mwanamke huyo amekuwa akipuuza mahitaji yake ya unyumba.

“Si mara ya kwanza Acen anamuumiza mumewe. Mwaka jana alimvunja mfupa wa bega wakati wanapigana na akakimbia. Shauri lilimalizika katika ofisi yangu na wakarudiana,” alisema.

Ogwal  alisema ulevi ndio husababisha ugomvi wa wanandoa katika eneo hilo.

Okot alipelekwa katika Kituo cha Polisi Olelpek kufungua kesi dhidi ya mkewe na kupelekwa katika hospitali ya Apac anakoendelea na matibabu.

Polisi wamesema shauri limefunguliwa na kupewa RB namba SD04/30/06/2019 na amepewa fomu ya polisi ya matibabu.

Mke amekimbia nyumbani baada ya tukio hilo.

Source: mwananchi