Magufuli amteua Mtatiro kuwa DC Tunduru

0
33
By Muyonga Jumanne, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, John Magufuli amemteua Julius Mtatiro kuwa mkuu wa Wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma.

Taarifa iliyotolewa leo Jumapili Julai 14, 2019 na mkurugenzi wa mawasiliano ya Rais Ikulu, Gerson Msigwa inasema Mtatiro amechukua nafasi ya Juma Homera aliyeteuliwa kuwa mkuu wa Mkoa wa Katavi.

Inaeleza kuwa uteuzi wa Mtatiro unaanza leo.

Mtatiro alikuwa naibu katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF), lakini alikihama chama hicho na kujiunga na CCM.

Source: mwananchi