Kizimbani kwa tuhuma za kukutwa na dawa za kulevya

0
37
By Suzana Otaigo na Alinda Kato, Mwananchi [email protected]

Dar es Salaam. Omari Said (40), mkazi wa Gongo la Mboto amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni kwa tuhuma za kusafirisha dawa za kulevya aina ya Heroin Hydrochloride.

Akisoma shtaka hilo leo Ijumaa Agosti 9, 2019 mbele ya hakimu, Caroline Kiliwa, wakili wa Serikali,  Neema Moshi amedai mshtakiwa alikamatwa Julai 16, 2019 na gramu 9.24 za dawa hizo eneo la Mwenge, jijini Dar es salaam.

Mshtakiwa huyo amekana tuhuma hizo huku wakili Moshi akidai upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika na kuomba tarehe nyingine kwaajili ya kutajwa.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 26, 2019 itakapotajwa tena.

Source: mwananchi