Kortini tuhuma za udhalilishaji wa kingono kwa binti wa miaka sita

0
36
By Alinda Kato na Suzana Otaigo, Mwananchi.

Dar es salaam, Mkazi wa Mikocheni ‘A’, Dar es Salaam nchini Tanzania  Thomas Mathias (34) amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni akikabiliwa na tuhuma za udhalilishaji wa kingono dhidi ya binti wa miaka sita.

Mshtakiwa huyo amefikishwa mahakamani hapo leo Ijumaa Agosti 9, 2019 na kusomewa shtaka linalomkabili na Wakili wa Serikali, Neema Moshi mbele ya Hakimu Caroline Kiliwa.

Wakili Moshi amedai mshtakiwa alifanya kosa hilo Juni 11, 2019 eneo la Mikocheni ‘A’ ambapo aliingiza vidole vyake sehemu za siri za binti huyo.

Mshtakiwa alikana tuhuma hizo na kusema kwa kusema ‘si kweli’.

Hata hivyo, Wakili Moshi amedai upelelezi wa shauri hilo bado haujakamilika na kuomba tarehe nyingine kwaajili ya kutajwa.

Hakimu Kiliwa akitoa masharti ya dhamana amesema mshtakiwa anapaswa kuwa na mdhamini atakayetakiwa kusaini bondi yenye thamani ya Sh200,000 ambapo Mathias  alikidhi vigezo na yuko nje kwa dhamana.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Agosti 27, 2019 itakapotajwa tena.

Source: mwananchi