Mtoto Daniel Evans atoweka nyumbani kwao Bunju A Dar es Salaam

0
26
By Baraka Samson, Mwananchi

Dar es Salaam. Mtoto anayefahamika kwa jina la Daniel Evans anadaiwa kutoweka nyumbani kwa wazazi wake leo tarehe 10 Agosti 2019 Saa 3:30 asubuhi.
Mtoto huyo anaishi Mtaa Simba eneo la Bunju A na wazazi wake.

Kwa mujibu wa baba mzazi,  Evans Rubara ameeleza kuwa, Daniel (12), ambaye ni mwanafunzi wa darasa la Saba shule ya Tuwapende watoto Nursery and Primary, aliondoka asubuhi lakini hakurudi tena nyumbani, hali iliyowashtua wazazi wake na kuanza kumtafuta siku nzima kwa marafiki zake bila mafanikio.

Inaelezwa kuwa mtoto huyo mwenye urefu wa futi 4.8, aliondoka nyumbani kwa wazazi wake akiwa amevaa fulana ya ndani yenye rangi ya maroon na rangi ya kijivu ubavuni ikiwa na maandishi ya Adidas juu yake, kaptura ya Jeans na viatu vyeusi vya kimaasai.

Familia hiyo imetoa taarifa katika kituo cha polisi cha Mbweni na kupatiwa RB namba  RB: WMB/2731/019

Familia inaomba kwa yeyote atakayepata taarifa za mtoto huyo kuwasiliana nao kwa namba za simu 0788-180-097 au 0688 832 600, ama kuripoti katika kituo cha polisi cha karibu.

Source: mwananchi