Polisi Texas wamsaka mwanamke mwizi harusini

0
29

Texas, Marekani. Polisi wanamsaka mwanamke ambaye amepachikwa jina la “mvamizi wa harusi” ambaye amekuwa akishutumiwa kuiba zawadi kutoka kwenye harusi kadhaa kusini mwa jimbo Texas nchini Marekani.

Mwanamke huyo ambaye hajatambuliwa amekuwa akishutumiwa kujitokeza kwenye harusi bila mwaliko na anadaiwa meshafanya hivyo katika harusi nne tangu Desemba.

Mtandao wa BBC umesema polisi wameushirikisha umma picha ya mwanamke huyo akiwa dukani akijaribu kutumia kadi ya zawadi, ambayo awali ilitumiwa na wanandoa waliofanya harusi karibuni.

Zawadi ya dola 4,000 (sawa na pauni 3,300) imetangazwa kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa zitakazosaidia kukamatwa kwake.

“Tusiache aharibu siku maalumu ya mtu yeyote na tumlete mvamizi huyu wa harusi za watu mbele ya sheria,” imesema taarifa ya mkuu wa polisi wa Comal – Texas.

Bodi ya maandalizi ya harusi katika eneo hilo imekiambia kituo cha habari cha CBS kuwa inatambua sura za watu waliopiga picha za harusi.

“Tumekuwa na harusi za wazi msimu huu wa majira ya joto ambao tumewaona wakizurura wakitafuta watu wanaouza bidhaa na kumbi za harusi,” amesema Rhonda Hollon, rais wa kampuni wa kampuni moja ya maandalizi ya harusi.

Bwana mmoja na mmewe waliliambia shirika la habari la NBC kuwa waligundua kwa mara ya kwanza kuwa wameibiwa zawadi wakati walipokuwa katika fungate yao.

“Ninafikiri tulipogundua kwa mara ya kwanza, lilikuwa ni jambo la kusikitisha lililotufanya tufikirie kwamba hili limetokea,” alisema Rittany Flores.

Yeye na mumewe Andy wanasema pia walimtambua mwanamke anayedaiwa kuwa mwizi, na wanaamini aliiba mamia ya dola taslimu na maelfu ya hundi za dola na kadi za zawadi.

Lakini wanandoa hao wanasema wanatumaini polisi wataweza kumpata muhusika wa uhalifu huo.

“Ninafikiri hilo ndilo tunalobaki nalo kutokana na hili, si kuacha tu yaishie hapa … Mvamizi wa harusi, kwa jina lolote wanalomuita, muondoshe katika siku yetu,” alisema Flores. “hawezi kuiba penzi letu.”

Source: mwananchi