Kamishna Jenerali Kasike afanya mabadiliko Jeshi la Magereza

0
20
By Elias Msuya, Mwananchi [email protected] [email protected]

Dar es Salaam. Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini Tanzania Bara, Phaustine Kasike amefanya mabadiliko ya wakuu wa Magereza wa mikoa mitatu.

Imeelezwa kuwa mabadiliko hayo yanalenga kuboresha utendaji kazi wa ndani ya jeshi hilo.

Taarifa iliyotolewa na msemaji wa Magereza SSP,  Amina Kavirondo jana Septemba 9, 2019 inaeleza kuwa aliyekuwa Mkuu wa Magereza Mkoa wa Geita, kamishna msaidizi, Robert Rumanyika amehamishiwa Magereza mkoani Kagera sehemu ya utawala na nafasi yake kuchukuliwa na aliyekuwa ofisa mnadhimi wa Magereza Mkoa wa Geita, Kamisha msaidizi wa Magereza (ACP) Edith Mbogo.

“Aliyekuwa Mkuu wa Magereza mkoani Rukwa, kamishna msaidizi wa Magereza AC, Jail Mwamgunda amehamishiwa mkoani Mtwara kuwa Ofisa mnadhimu wa mkoa na nafasi yake imechukuliwa na mkuu wa Gereza Mkwaya, Kamishna msaidizi Magereza (ACP), Marco Kilumbo.”

“Aliyekuwa mkuu wa Magereza Mkoa wa Katavi, kamishna msaidizi wa Magereza (ACP), Alexander Mmassy amehamishiwa Magereza Mkoani Njombe kuwa ofisa mnadhimu wa Mkoa na Nafasi yake kuchukuliwa na mnadhimu wa Magereza mkoani Ruvuma, ACP Wilson Mwansomola,” amesema.

Advertisement

Source: mwananchi