Davido amvisha pete ya uchumba Chioma

0
20
By Elizabeth Edward, Mwananchi

Nyota wa muziki wa Nigeria, Davido anaelekea kuachana na kambi ya ukapera baada ya kumvisha pete ya uchumba mpenzi wake Chioma.

Wawili hao wamekuwa kwenye uhusiano kwa muda mrefu na sasa wameamua kuupeleka uhusiano huo katika hatua nyingine.

Kupitia kurasa zao za Instagram wameweka picha ya kidole kilichovalishwa pete ya almasi inayoonekana kuwa ya thamani.

Kabla kuvishana pete wiki chache zilizopita, Davido na Chioma walikuwa na hafla ya kuzikutanisha familia zao kwa ajili ya utambulisho.

Taarifa zilizopo ni kwamba wanatarajia kufunga ndoa mwakani nchini Nigeria.

Advertisement

Source: mwananchi