Rais Magufuli kupokea taarifa mabilioni ya wahujumu uchumi

0
30
By Mwandishi Wetu, Mwananchi

Dar es Salaam. Rais wa Tanzania, John Magufuli leo Jumatatu Septemba 30, 2019 atapokea taarifa ya utekelezaji wa ushauri alioutoa wa kuwasamehe watuhumiwa wa uhujumu uchumi walio tayari kutubu na kurejesha fedha na mali.

Mkurugenzi ya Mawasiliano ya Rais Ikulu ya Tanzania, Gerson Msigwa amesema, “DPP atawasilisha taarifa leo Septemba 30, 2019 saa 3:30 asubuhi Ikulu Jijini DSM. Fuatilia Redio, TV na Mitandao.”

Septemba 22, 2019 Rais Magufuli alipokuwa akiwaapisha viongozi mbalimbali aliowateua, alitangaza siku saba kwa watuhumiwa wa mashtaka ya uhujumu uchumi na utakatishaji fedha ambao watakuwa tayari kukiri makosa na kulipa fedha wanazodaiwa kuachiwa.

Siku saba ilikuwa kuanzia Septemba 23 hadi 28, 2019 ambapo watuhumiwa hao walitakiwa kuwasilisha maombi yao kwa Mkurugenzi wa Mashtaka Tanzania (DPP).

Source: mwananchi