Bunge la Marekani laamuru Ikulu ya Trump kutoa nyaraka za mawasiliano na Ukraine

0
36

Washington. Kamati za Bunge la Marekani zinazoendesha uchunguzi dhidi ya Rais Donald Trump zimeiamuru Ikulu ya White House kuwasilisha nyaraka zote za mawasiliano kati ya Trump na Ukraine.

Amri hiyo imetolewa baada ya Ikulu ya Marekani kushindwa kuchapisha kwa hiari nyaraka hizo kabla ya kumalizika muda wa mwisho uliokuwa umetolewa wa hadi Ijumaa.

Mmoja wa viongozi wa Kamati za Bunge la Marekani, amesema ni wazi Rais Trump amechagua njia ya kuficha ukweli baada ya kushindwa kwa mwezi mzima kuweka wazi nyaraka za mawasiliano yake na Ukraine.

Hapo jana, Trump alisema huenda asitoe ushirikiano kwenye uchunguzi dhidi yake ambao unahusu madai kwamba alimshinikiza Rais wa Ukraine kumchunguza makamu wa rais wa zamani, Joe Biden na mwanawe kwa tuhuma rushwa.

Shinikizo hili linadaiwa kutolewa wakati ambapo Marekani ilikuwa inashikilia msaada wa dola 400 milioni uliokuwa tayari umeidhinishwa kwa ajili ya Ukraine.

Inachunguza kama kuna uhusiano baina msaada huo na uchunguzi uliokuwa unashinikizwa.

Advertisement

Source: mwananchi