Waziri mkuu Ethiopia ashinda tuzo ya amani ya Nobel

0
15

Waziri mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed ameshinda tuzo ya amani ya ‘Nobel’ kwa mwaka 2019.

Waziri mkuu huyo ametunukiwa tuzo kutokana na  jitihada zake kuleta amani na ushirikiano wa kimataifa. Ametajwa kuwa mshindi wa 100 wa Nobel huko Oslo, Norway.

Kikubwa kilichochangia tuzo hiyo ni mkataba wa amani uliosainiwa mwaka jana na kumaliza mgogoro wa kivita na nchi jirani ya Eritrea uliochukua miaka 20.

Jumla ya washiriki 301 waliochaguliwa katika tuzo hizo zenye hadhi kubwa duniani, washiriki 223 ni watu binafsi na kampuni 78 .

Kwa mujibu wa BBC, tayari watu walikuwa wamekisia nani angeshinda tuzo hiyo. Chini ya kanuni za asasi ya Nobel. Washiriki waliotajwa majina yao hayaruhusiwi kuchapishwa kwa miaka 50.

Tuzo hizo zilianzishwa mwaka 1895 na mwanasayansi wa Sweden, Alfred Nobel kwa mapenzi yake na  kila mwaka hutolewa tuzo tano, kwenye Kemia, fasihi andishi, tuzo ya amani, Fizikia na Fiziolojia (Dawa).

Advertisement

Abiy Ahmed ni nani?

Baada ya Ahmed kuwa waziri mkuu Aprili 2018, Abiy alianzisha mabadiliko nchini Ethiopia ambako unyanyasaji na ukiukaji wa haki za binadamu ulikuwa umetamalaki.

Ahmed aliwaachia huru maelfu ya wanaharakati waliokuwa gerezani na wale walio uhamishoni kwaliruhusiwa kurejea nyumbani.

Kwa nini ameshinda

Kamati ya tuzo hiyo ya Norwal katika hutuba yake, ilisema Abiy ametunukiwa tuzo hiyo ya heshima kwa kufanikiwa kutatua mgogoro wa mipaka na nchi jirani ya Eritrea.

“Tuzo hiyo ina maana kuwa imetambua juhudi za washirika wanaotaka amani na makubaliano nchini Ethiopia, Afrika Mashariki na Afrika kwa ujumla,” walisema.

Source: mwananchi