Malawi yatangaza corona janga la kitaifa

0
30

Facebook

Twitter

Google+

Pinterest

WhatsApp

Telegram

Lilongwe, Malawi

Rais wa Malawi, Lazarus Chakwera amelitangaza corona kuwa janga la kitaifa kutokana na kuongezeka kwa kasi kwa maambukizi ya virusi vya nchini humo.

Katika hotuba maalum kwa taifa hapo jana, Rais Chakwera amesema, kufuatia ongezeko kubwa la vifo na maambukizi mapya ya virusi vya Corona, ataitisha mkutano wa dharua kujadili hatua zijazo za kinga na udhibiti.

Pia ametoa wito kwa Jumuiya ya kimataifa kuongeza misaada kwa Malawi ili kuisaidia kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazotokana na janga la COVID-19.

Source: mtanzania.co.tz