Aliyetaka Waziri Mkuu achunguzwe afutwa kazi

0
59

HATIMAYE Waziri Mkuu wa Haiti, Ariel Henry, amemwandikia barua Mwendesha Mashitaka Mkuu nchini humo,  Bed-Ford Claude, akiwambia anatakiwa kukiachia kiti hicho.

Hatua hiyo imekuja baada ya Claude kutaka Waziri Mkuu huyo achunguzwe kutokana na mauaji ya Rais Jovenel Moise aliyeuawa Julai 7, mwaka huu.

Katika barua ya ‘kumtumbua’ ambayo Waziri Henry amemwandikia Claude, amemwambia: “Nina furaha ya kukuarifu kwamba imeamuliwa kusitisha kibarua chako.”

Kwa inavyoeleweka, Waziri Mkuu wa Haiti hawezi kuwajibishwa na chombo chochote zaidi ya Rais lakini kwa sasa nafasi hiyo haina mtu baada ya Moise kuuawa akiwa nyumbani kwake.

Source: mtanzania.co.tz