Becker, Fabinho nje Liverpool

0
69

MERSEYSIDE, England

LIVERPOOL huenda ikawakosa kipa Alisson Becker na kiungo Fabinho katika mchezo wa wa Jumamosi ya wiki hii dhidi ya Watford.

Si kwamba ni majeruhi, bali wawili hao wako na Brazil na wana mechi ya Ijumaa, hivyo ni ngumu kurudi mapema England na kutapata muda wa kutosha kujiandaa na mechi hiyo ya Ligi Kuu.

Mbali ya hilo, pia presha kwa kocha Jurgen Klopp ni kwamba bado hana uhakika wa kumuona Diogo Jota akiwa fiti kwa ajili ya mtanange huo kwani Mreno huyo alipata majeraha ya misuli akiwa na kikosi cha Ureno.

Habari njema kwa Liverpool inayoshika nafasi ya pili kwenye msimamo, ni kurejea kikosini kwa nyota tegemeo kikosini, Trent Alexander-Arnold.

Source: mtanzania.co.tz