‘Nilikimbia ukame wa makombe Arsenal’

0
53

BEKI wa pembeni raia wa Hispania, Hector Bellerin, amesema aliamua kuondoka Arsenal na kujiunga na Real Betis ili atimize ndoto yake ya kutwaa mataji.

“Nilitaka jua na joto (lililoko Hispania) lakini sikuja hapa kutembea, nimekuja kupambania nafasi ya kucheza. Nimeondoka Arsenal ili nitwae mataji na Real Betis. Siko hapa kupumzika,” amesema.

Bellerin aliyecheza mechi 239 akiwa na ‘uzi’ wa Arsenal, atavaa jezi namba 19 kwa kipindi chote atakachokuwa na kikosi cha Betis.

Washika Bunduki waliinasa saini yake akiwa kinda, ambapo walimtumia kwenye ‘academy’ yao kuanzia mwaka 2011 na ameondoka akiwa ameipa mataji matatu ya FA (2015, 2017 na 2020).

Source: mtanzania.co.tz