Pyramids kutua kesho

0
82

Na Mwandishi Wetu

WAPINZANI wa Azam FC, kikosi cha timu ya Pyramids kutoka Misri kinatarajia kutua kesho nchini kwa mchezo wao wa Kombe la Shirikisho Afrika utakaopigwa Oktoba 16,2021 kwenye Uwanja wa Azam Comlex, jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Klabu ya Azam, Thabit Zakaria ‘Zaka Zakazi’, amesema Pyramids itawasili saa tatu usiku na itafanya mazoezi kwa siku mbili  Oktoba 14 na 15 katika uwanja huo.

Akizungumzia maandalizi ya kikosi chao, amesema yanakwenda vizuri na mikakati ya ushindi inaendelea kuhakikisha miamba hiyo ya Misri inapigika.

“Mwalimu anaendelea kufanyia kazi kasoro zilizojitokeza katika michezo iliyopita, wachezaji wote waliokuwa timu ya Taifa wamerejea hakuna majeruhi zaidi ya Prince Dube ambaye tangu zamani anajulikana ni majeruhi.

“Mikakati ya ushindi kwa upande wa kiufundi yanafanyika, hii ni kupitia mazoezi yanayofanyika na mwisho wa siku tutajua ni namna gani wanaweza kupigika Pyramids,” amesema Zaka Zakazi.

Source: mtanzania.co.tz