Waliotoroka gerezani wakamatwa

0
62

WAFUNGWA 108 kati ya 240 waliotoroka gerezani nchini Nigeria wamerejea kwenye mikono ya vyombo vya dola.

Taarifa hiyo inakuja baada ya kile kilichotokea mwishoni mwa wiki iliyopita, ambapo watu wenye silaha walivamia gereza katika Jimbo la Kogi na kutorosha wafungwa.

Licha ya kutofahamika, inasaidikiwa kuwa ni sehemu ya vikundi vya kihalifu vilivyotawala maeneo mbalimbali, hasa Kaskazini-Magharibi mwa Nigeria.

Katika tukio hilo la kuvamia gereza, wahalifu walisababisha vifo vya wanausalama wawili.

Source: mtanzania.co.tz